Friday, February 3, 2012

Furaha Maugo


SHABAN Abdallah(27) mkazi wa Gongo la Mboto Mzambaurauni, jijini Dar es salaama anawaomba  wasamaria wema kujitokeze kumchangia fedha kwa ajili ya operesheni ya kukatwa mguu unaomsumbua kwa  takribani miaka kumi sasa.
Akizungumza jijini Dar es salaam katika ofisi za gazeti hili zilizopo Tabata reline, Abdallah  alisema anahitaji jumla ya Sh500,000 hadi 700,000 kwa ajili ya kulipia gharama za operesheni ya kukata  mguu mmoja wa kulia unaoonekana kuathirika kutokana na matende  matende.
“Nimesumbuka na kuwa mtu wa kulia kila siu  kutokana na maumivu ya  mguu huu kwa takribani miaka kumi sasa,nimetumia kila aina ya dawa bila mafanikio badala yake mguu unazidi kujaa maji kila kukicha hali inayonisababishia kupata  maumivu makali kiasi kwamba wakati mwingine nashindwa kutembea”alisema Abdalla.

Na kufafanua kuwa alianza kuumwa mguu huu mwaka 2001 kwani ulianza kwa  dalili za kuwasha lakini kadri siku zinavyoendelea  na  mguu unazidi kuvimba na kumsababishia maumivu makali.

Hivyo basi kutokana na hali hiyo Shaban alisema inamlazimu kukaa tu nyumbani na kwasasa hana kitu chochote kinachomuingizia kipato wala mtu anayemtegemea  kukidhi mahitaji yake ya kila siku wala  gharama za matibabu.

‘Mi nadhani suluhisho pekee la mguu huu ni kukatwa na hivi sasa nipo tayari kwa zoezi hili ninachoomba tuwasamarai wema wajitokeze kunichangia fedha a kukijikimu katika operesheni hiyo nikiamini baada ya kupona nitafanya shughuli zangu vizuri”alisema Shabani.

Na kueleza kuwa, Agosti mwaka jana alivyoenda  katika  hospitali ya Ocean Road ndio aligundulika kuwa na matende  na dawa yake ni operesheni ya kupunguza maji au kukatwa mguu kabisa, lakini kutokana na maumivu anayopata ameamua ukatwe kabisa hivyo anawasihi wasamiria wema wamchangie kwa chochote kufanikisha zoezi hilo.

“Gharama za operesheni ya kukata mguu huu  hospitali ya Muhimbili nimeambiwa ni Sh 200,000, kipimo cha damu ya usiku  Sh 15,000 ,gharama za  kupigwa Ultra Sound(Mionzi )ni shilingi 35,000” alisema Abdalla na kufafanua kuwa anaamini kiasi hicho alichoomba kitakidhi mahitaji yake kwa sasa.
Kwa yeyote aliyegushwa na jambo hili anaweza kuwasiliana na Shabani kwa namba 0712 235060 au kumtumia pesa kwa njia ya tigo pesa

No comments:

Post a Comment